Wednesday, August 8, 2012

PREZZO AAMBULIA KIDUCHUU BIG BROTHER 2012

RAPA wa Kenya, CMB Prezzo (pichani kushoto) ameibuka mshindi wa pili wa shindano la Big Brother StarGAME 2012 huku akimshuhudia kijana wa nyumbani Keagan akizibakisha kwa mara ya kwanza dola 300,000 (sawa na Sh. milioni 460) nchini Afrika Kusini.
Washiriki sita walikuwa wamebaki ndani ya nyuma mbapa leo siku ya 91 na ya mwisho ya shindano hilo, Kyle wa Uganda, Wati (Malawi), Lady May (Namibia), Talia (Zambia), Prezzo na Keagan.
Wati alitangulia kutolewa, akafuatia Kyle, Talia, Lady May na wakabaki wawili tu ndani ya jumba Prezzo na mwenyeji wa mashindano, Keagan.
Baada ya kusubiri kwa muda mrefu huku burudani zikiendelea nje ya jumba, mtangazaji wa shoo hiyo, IK, alirejesha kamera ndani ya nyumba na baada ya kuwaweka roho juu washiriki hao wawili ikiwa ni pamoja na kuwataka waseme maneno…
RAPA wa Kenya, CMB Prezzo (pichani kushoto) ameibuka mshindi wa pili wa shindano la Big Brother StarGAME 2012 huku akimshuhudia kijana wa nyumbani Keagan akizibakisha kwa mara ya kwanza dola 300,000 (sawa na Sh. milioni 460) nchini Afrika Kusini.
Washiriki sita walikuwa wamebaki ndani ya nyuma mbapa leo siku ya 91 na ya mwisho ya shindano hilo, Kyle wa Uganda, Wati (Malawi), Lady May (Namibia), Talia (Zambia), Prezzo na Keagan.
Wati alitangulia kutolewa, akafuatia Kyle, Talia, Lady May na wakabaki wawili tu ndani ya jumba Prezzo na mwenyeji wa mashindano, Keagan.
Baada ya kusubiri kwa muda mrefu huku burudani zikiendelea nje ya jumba, mtangazaji wa shoo hiyo, IK, alirejesha kamera ndani ya nyumba na baada ya kuwaweka roho juu washiriki hao wawili ikiwa ni pamoja na kuwataka waseme maneno yao ya mwisho shindanoni, baadaye akamtangaza Keagan kuwa ndiye mshindi.
Prezzo hakupoteza muda wala hakukumbuka kwenda kumpongeza mwenzake, alitoka moja kwa moja nje ya jumba, ambako alipokewa na nderemo za mashabiki waliojaa pamoja na mtangazaji IK.
Huku akijitahidi kuzuia machozi yasitoke, 'The Prezident himself' Prezzo aliuliwa kama ataendeleza mapenzi yake na muimbaji wa Nigeria, Goldie, kama walivyokuwa mjengoni, alijibu: "Tusibiri tuone."
Kisha Prezzo aliambiwa kuwa hataondoka mtupu kwa sababu kura za mashabiki zimemchagua kuwa balozi wa kampeni ya ONE ambayo inawajumuisha mastaa kama rapa Nas, Mary J. Blige wa Marekani na wengine wengi.
"Mbali na hiyo pia umealikwa kwenda kuhudhuria shoo ya Jay Z Marekani," alisema IK kumweleza Prezzo.
IK pia aliwaambia washiriki wengine walioshika nafasi tano za kwanza: "Hamtaondoka mikono mitupu... nyota mtapata PVR decoder, IPhone smartphone, na scooter."
LIcha ya ushindi, Keagan alionekana kuwa mtulivu mno, hakushangilia, pengine alikuwa haamini kama sasa yeye ni tajiri wa Sh. milioni 460.

No comments:

Post a Comment