Sunday, September 2, 2012

Msanii wa muziki wa dansi anayekipiga kwenye bendi maarufu ya muziki huo Mashujaa Band, Chalz Baba, amedai kuwa yeye ni mfanyabiashara wa muziki hivyo anapoona sehemu aliyopo haina manufaa kwake lazima andoke na anaamini hii si upande wake pekee hata kwa wamiliki nao wanapoona msanii hana faida kibiashara wanamfukuza.

Kauli za msanii huyo zinaonesha kuwa hafanyi muziki kwa upendo wake bali anafanya kwa ajili ya maslahi binafsi kwanza na ndiyo maana
wasanii wengi wa muziki wa dansi wanashindwa kuwa maendeleo zaidi badala yake wanahama hama bendi ili kutafuta maslahi ambayo hayaji bila kuonesha kiwango katika uimbaji au upigaji wa vyombo.

Chalz Baba alidai kuwa kikubwa anachokifanya si kutafuta hela pekee pale hata kujenga heshima ya jina lake kupitia muziki huo kwani anaamini hiyo ndiyo njia pekee ya kumfanya awe msanii lulu katika tasnia hiyo ya muziki wa dansi Tanzania.

Hata hivyo alipoulizwa kuwa mashabiki wake hawaamini kiwango chake na inaonekana kuwa amepata umaarufu bada ya kutoka na Wema Sepetu kimapenzi, alijibu kuwa kila mtu anamtazamo wake na yeye hafanyi kwa sababu mtu fulani kazungumza.

No comments:

Post a Comment