Friday, June 29, 2012

Camp Mulla wajiunga na kampeni ya kupambana na njaa Africa Magharibi


Kundi la hip hop la nchini Kenya, Camp Mulla limeungana na kundi maarufu la duniani la muziki wa rock kutoka Uingereza Coldplay katika kampeni ya shirika la umoja wa mataifa la Oxfam ya kupambana na baa la njaa kwenye eneo la Sahel, Afrika Magharibi.
Camp Mulla ambao hivi karibuni walitajwa kuwania tuzo za BET, wameamua kutumia umaarufu wao walioupata kwa haraka duniani kwa kujihusisha na masuala ya kibinadamu.
Katika kampeni hiyo mwanamuziki wa Nigeria Ice Prince naye ameungana na Coldplay pamoja na Campmulla.
Karibu watu milioni 18.4 wanadaiwa kukumbwa na uhaba wa chakula,huku milioni 6 wakiwa hawana kabisa chakula.
Coldplay, kundi ambalo bila shaka kwa sasa ni kubwa zaidi la rock duniani limekuwa mstari wa mbele kuliangalia suala la njaa huko Sahel, eneo linalojumuisha nchi nane kuanzia Chad hadi Senegal.
Ice Prince aliandika kwenye mtandao wa Twitter kuhusa majukumu hayo na kuahidi kutoa support; “As a West African Artiste, I’m really glad to be supporting the @Oxfam Beyond BET: Sahel Hunger crises!! We want change!”
Kwa mujibu wa shirika la kuhudumia watoto duniani,Unicef zaidi ya watoto milioni moja walio chini ya miaka mitano huko Sahel wanakabiliwa na utapiamlo mkali.
Kutokana na njaa hiyo, wakulima wapo njia mpanda kuhusu kula ama kuzitunza mbegu zao kwaa ajili msimu ujao wa kilimo, huku wengine wakianza kula matunda mwitu.

No comments:

Post a Comment