Tuesday, June 19, 2012

HUU NDIO MKOKO WA DIAMOND, KITU MILLION 60

Staa wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’ amevuta mkoko wa Kijanja wenye thamani ya ‘mkwanja wa Kibongo Milioni 60 keshi. Akizungumza na blog hii muda mfupi baada ya kupokea ‘dinga’ hiyo aina ya Land Cruiser Prado TX kutoka kwa wakala aliyekuwa akishughulikiwa mpango mzima wa kuingia kwake hapa Bongo, Diamond alifunguka kuwa alikuwa na mpango wa kuvuta mkoko ‘dizaini’ hiyo kitambo lakini kuna mambo kadhaa yakawa yanachelewesha. ‘Ndinga’ hiyo aina ya Land Cruiser Prado TX kutoka kwa wakala aliyekuwa akishughulikiwa mpango mzima wa kuingia kwake hapa Bongo, Diamond alifunguka kuwa alikuwa na mpango wa kuvuta mkoko ‘dizaini’ hiyo kitambo lakini kuna mambo kadhaa yakawa yanachelewesha. “Nashukuru Mungu kuwa mpango wangu umetimia, nilipanga hivi kitambo lakini kuna baadhi ya mambo yalichelewesha hatua hiyo, najua watu watasenama mengi kuhusu hili lakini ukweli ni kuwa huu ni mchuma wangu” alisema Diamond. Katika hatua nyingine Diamond alifunguka kuwa awali alinunua mdinga kama hiyo huko visiwani Zanzibar, lakini baada ya kuikagua aligundua kuwa lina matatizo na kuamua kulirudisha na kuagiza kitu kipyaaaaaa.

No comments:

Post a Comment