Friday, June 22, 2012

MWANAMUZIKI HUSSEIN MACHOZI AMETANGAZA KUAMIA KENYA


Mwanamuziki wa Tanzania aliyetamba na vibao kama ‘Kwaaajili Yako’ na ‘Full Shangwe’ Hussein Machozi, amesema anafikiria kuhamia kabisa Kenya kwakuwa anahisi muziki wake unathaminiwa zaidi huko kuliko nyumbani.
Akijibu swali  lililotaka kufahamu kama ana mpango huo kwakuwa ni muda mrefu sana sasa amekuwa akiutumia nchini Kenya kuliko Tanzania, Machozi alisema,”Yap naona pananifaa sana kwa muziki wangu ambao hauna unafiki si unajua watu wa huku sio wanafiki.”
Kwanini anasema Tanzania kuna unafiki? “Okay, watu wa media hawako free kabisa yaani huwa wanafuata upepo wanapoanzisha wale wenye nguvu. Yaani wakitaka kumtoa mtu wao na media zingine zinafuata wala hawashtuki kuwa analazimishwa atoke, wakati kuna ngoma kibao kali wanazipotezea ili mtu wao apite. Matokeo yake wanatoaga ngoma moja inahit baada ya hapo ni pumba tupu. Huwa inaniuma sana.”
“Kwa kenya mambo hayo hakunaga asee! Huku kama ngoma ni kali basi itatandikwa hadi noma, ila kama ni mbaya huwezi hata kuiskia. Nakubalika huku coz ngoma zangu ni kali na zina kichwa na miguu namaanisha wimbo uko na story ya kufuatilia na inaskilizika na rika zote, nadhani hii ni sababu tosha sana,” alisema Machozi.
Msanii huyo tayari ameshafanya ngoma na wasanii wa Kenya wakiwemo Habida,Size 8 na DNA

No comments:

Post a Comment