Wednesday, July 18, 2012

NDOA YA HEMED YAKAMWA, KISA ELIMU NDOGO

NDOTO kufunga pingu za maisha siku za karibuni alizokuwanazo nyota kutoka 'Bongo moive' Hemed Suleiman 'PHD', zimeota mbawa kufuatia wazazi wa mlimbwende aliyetaka kumuoa kuweka ngumu. katika mahojino ya dakika kadhaa aliyofanya Hemed amesema kuwa tayari alikuwa ameanza taratibu za kushughulikia ndoa yake na mrembo huyo iliyopangwa kufungwa kimya kimya kwa kuogopa watu wenye nia mbaya lakini amejikuta akilazimika kustisha harakati hizo kufuatia wazazi wa binti huyo wakaweka ngumu kwa madai kuwa wanataka mtoto wao amalize kwanza masomo yake na kupata 'mastaz' kwa kuwa elimu ya Degree aliyonayo hivi sasa wanahisi bado haijamtosha. "unajua mchumba wangu hivi sasa ana elimu ya degree hivyo wazazi wamesema kwao hiyo bado ni elimu ndogo hivyo hawezi kuruhusu jambo hilo kwanza mpaka apate 'mastaz' halafu ndiyo mambo mengine yatafuata, imeniuma sana kwa kuwa wenyewe tulishakubaliana na mwenzangu alikuwa tayari kwa hilo" alisema Hemed. katika hatua nyingine Hemed ameiambia teentz.com kuwa yuko katika hatua za mwisho kutoa muvi yake mpya aliyoibatiza jina la Mererani ndani yake akiwa amemshirikisha swahiba wake wa kitambo Yusuf Mlela sambamba na wakali wengine kibao wanaofanya kweli na Bongo movie wakati huo huo nyota huyo amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula tayari kwa ujio wa ngom ayake mpya iliyopewa jina la Mama Kimbo sambamba na video yake ambayo soon itakuwa hewani kupitia teentz.com.

No comments:

Post a Comment