Sunday, August 26, 2012

AVRIL AMKOSA LINEX WA IFOLA

 
Saku za hivi karibuni kupitia chanzochetu cha habari tuliwafahamisha kuhusu Ujio wa KEKO na nia yake ya kufanya ngoma na wakali wa Bongo kama Hamisi mwinjuma na Farid Kubabanda i mean FA&FQ.Mkali huyo toka 256 alisema kua Chaguo lake la kwanza ni FA.

Sasa leo madivas wawili wa 254 watakua Club Billcanas hapa nawazungumzia madivaz wanaotamba na ngoma ya Chokoza Avril na Marya.
Kitu kimoja chanzo chetu cha habari kilitaka kukifaham kutoka kwa Avril Je anataka kufanya ngoma na mkali gani hapa Tanzania Bongo land kwa Baba Ridhwani.Avril bila kuficha alimtaja kijana toka Kigoma ambae amesikika katika Chorus ya Leka Dutigite Linex kua ndio chaguo lake la kwanza.

Bahati mbaya iliyopo kua wakati leo ndio siku ya Show Linex nae atakua Kigoma katika harakati zake za kikazi kuna uwezokano mkubwa 90% ya kutokuwepo kwa kolabo hilo kati ya Avril & Linex.

No comments:

Post a Comment