Monday, August 27, 2012

BREAKING NEWS....RC NJOMBE AIBIWA,ASKARI WALIOKUWA LINDONI MATATANI

                                                     RC   Njombe Aser Msangi

Watu wasiofahamika wameingia nyumbani kwa mkuu wa mkoa wa
Njombe [RC] Kaptain Mstaafu Asseri Msangi usiku wa kuamkialeo na kuiba vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milionimoja.
Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com mkoani Njombe Gabriel Kilamlya Kaptaini Msangi alisema tukio hilo lilitokea usiku wa manane wakati

amelala, na alivitaja vitu vilivyoibiwa kuwa ni pamoja na kidadavuo

mpakato [laptop] yenye thamani ya shilingi laki saba na nusu pamoja

na simu tatu za vijana wake zenye thamani ya shilingi ya laki nne na
nusu.


Hata hivyo Kaptaini Msangi alisema tukio hilo limemsikitisha sana

hasa ikizingatiwa kwamba nyumba yake inalindwa na askari wa jeshi

la polisi wenye bunduki zenye risasi za kutosha.


"Nimeishi miaka mingi kwenye nyumba bila ulinzi wowote nilipo

kuwa mkuu wa wilaya [DC] sijawahi kuibiwa lakini leo hii mkuu wa

mkoa nina walinzi lakini nimeibiwa, mpaka hapa naona haina haja ya

kuwa na walinzi"alisema Msangi.


Aidha Msangi alisema anawatilia shaka askari polisi waliokuwa zamu

huku kuwa wanahusika na tukio hilo.


Mkuu huyo wa mkoa aliongeza kuwa wakati mwingine walinzi hao

huwa wanatoroka lindo na kwenda kunywa pombe.


Kufuatia tukio hilo jeshi la polisi mkoani Njombe linawashikilia

askari wawili wa jeshi hilo waliokuwa lindo kwa mkuu wa mkoa

usiku huo wa tukio kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Akizungumza na mtandao huu kamanda wa jeshi la polisi mkoani

Njombe Fulgency Ngonyani aliwataja askari hao kuwa ni pamoja na

askari mwenye namba G. 5414 PC Ombeni na askari mwenye

namba G. 5455 PC Mohamed ambao wakati tukio hilo likitokea ndio

waliokuwa zamu ya kulinda kwa mkuu huyo wa mkoa.

"Tunawashikilia askari hawa kwa kuwa ndio walikuwa lindo, lakini

hata hivyo tumefanya uchunguzi wa awali hatujaona sehemu yoyote

iliyobomolewa yawezekana watu walifanya tukio hilo la wizi

walitumia funguo bandia" alisema Kamanda Ngonyani.

Akizungumzia hataua ya askari wa jeshi hilo kuwa na tabia ya

kuacha lindo na kwenda kunywa pombe, Kamanda Ngonyani alisema

hana taarifa hizo lakini aliahidi kulifanyia kazi, ambapo amemwagiza

mkuu wa upepelelezi kufanya uchunguzi juu ya jambo hilo.

No comments:

Post a Comment