Friday, June 15, 2012

BET AWARDS 2012: Camp Mulla Waomba Kura za wana Afrika Mashariki

Zikiwa zimesalia siku 16 tu kabla ya kufanyika kwa tuzo za BET mwaka 2012, kundi la vijana watano kutoka Kenya, Campmulla limewaomba wapenzi wa muziki wa Afrika Mashariki kuwapigia kura. Kundi hilo limetajwa kuwania kipengele cha Best International Act Afrika likishindana na wasanii kama Ice Prince, WizKid wa Nigeria, Sarkodie wa Ghana, Lira wa Afrika Kusini na Makobe wa Mali. Ni mara ya kwanza kwa msanii ama kundi la Afrika Mashariki kutajwa kwenye tuzo hizo. Tuzo za BET zitatolelwa July 1, na host atakuwa muigizaji mkongwe wa filamu Samuel L Jackson. Leo kundi hilo kupitia Facebook limeandika, “ Support the Camp Mulla Movement and keep sharing; http://www.bet.com/topics/c/camp-mulla.html.” Wasanii watakaotumbuiza mwaka huu ni pamoja na Usher, Chris Brown, Nicki Minaj, Big Sean na 2 Chainz. Add a comment

No comments:

Post a Comment