Friday, June 15, 2012

Video ya Party Zone, Ay feat. Marco Chali

Hatimaye imetoka baada ya kusubiriwa kwa muda mrefu. Check it out! Sasa tumepata jibu la kwanini video hii imemgharimu milioni thelathini na ushee. Hii ni video ambayo kila kituo kikubwa cha runinga kitataka kiwe nayo. Jana Trace ya Ufaransa imekuwa ya kwanza kuicheza. Kwenye video hii AY kaonesha uwezo mzuri zaidi katika kuimba pengine kuzidi nyimbo nyingi ama zote alizowahi kuimba. Party zone ni zile nyimbo ambazo huingia kichwani kwa mtu haraka na kujikuta akiuimba kimya kimya bila kuwa na taarifa. Ni ngoma ambazo zikipigwa Club huwezi kuvumilia kukaa zaidi ya kuinuka na kulishambulia stage. Kwenye wimbo huo Marco Chali ameonesha kwa urefu zaidi uwezo wake wa kuimba tofauti na jinsi tulivyomzoea kwenye nyimbo za awali ambazo mara nyingi aliimba chorus peke yake. Ngoma hii imetoka katika kipindi ambacho nyimbo za aina hii ya dance zinafanya vizuri mno duniani. Ni wimbo wa biashara zaidi na tuna uhakika utampeleka mbali sana. Marco Chali pia ajiandae kuanza kutafutwa na wasanii wengi duniani kwa kazi hii nzuri ya mikono yake. Video hii tunaipa mic tano. Watoto wazuri pia, Big up AY

No comments:

Post a Comment