Friday, June 15, 2012

NDOA YA H-BABA, FROLA UTATANdoa ya nyota wanaotamba kupitia fani ya muziki na filamu Bongo, Hamis Ramadhan Baba, ‘ H-Baba’ na Frola Mvungi, bado iko gizani kufuatia, kijana huyo kushindwa kufikia uamuzi. Akizungumza ‘live’ na mtandao namba moja kwa stori za mastaa (Teentz.com) H-Baba amesema kuwa hana uhakika kama jambo hilo linaweza kupewa nafasi hivi sasa kwa kuwa kuna mambo mengi yanyomfanya kushindwa kufikia uamuzi wa kufunga ndoa na mwigizaji huyo “Bado kuna utata, sijafikia uamuzi wa kufanya jambo hilo hivi sasa, sitaki kusema sana kwa sababu najua kuna watu ambao wanajaribu kuingilia uhusiano huu, ki ukweli sijafikia uamuzi kuna mambo madogo madogo bado nayachunguza kwa mwenzangu na wakati ukiwadia basi kila kitu kitakuwa wazi” alisema H-Baba aliyeingia kwenye uhusiano na Frola mwaka mmoja uliopita.

No comments:

Post a Comment