Thursday, June 14, 2012

DOGO JANJA BAADA YA KUTIMULIWA TIPTOP Siku moja baada ya Dogo Janja kudaiwa kufukuzwa Tip Top Connection, ukweli halisi kuhusiana na uamuzi huo umewekwa wazi na yeye mwenyewe. Sababu zilizotajwa na Tip Top Connection ni kwamba Dogo Janja alilewa sifa na kuwa mtoro shuleni. Baada ya kuwasiliana nae kwa njia ya simu saa moja asubuhi leo (June 14) akiwa stand kurejea nyumbani, uonevu na dhuluma ndivyo vilivyomchosha kuishi Dar es Salaam. Anasema tangu aje Dar es Salaam hajawahi kusaidiwa chochote na Madee zaidi ya mambo ya muziki pekee huku kula, malazi na ada ya shule vikifanywa na rafiki yake Madee aitwaye Abdallah Doka ambaye (Dogo Janja) alikuwa akiishi kwake. Anasema kutokana na ngoma zake kujipatia umaarufu alikuwa akipata show nyingi nchini na zote alikuwa halipwi chini ya milioni moja. Kilichokuwa kinamsikitisha anasema ni kulipwa hela kidogo isiyozidi laki mbili na hivyo kumfanya aishi kwa tabu licha ya kuingiza hela nyingi za show. “Nilikuwa navumilia tu bro kwasababu kila nilipolalamika kuhusu mambo ya hela Madee alikuwa mkali sana,” alidai D Janja Dogo anasema ilikuwa inafikia wakati akifanya show za ukumbuni hulipwa elfu hamsini au chini ya hapo na wakati mwingine alikuwa halipwi kabisa. Tamaa ilizidi kumwingia Madee kiasi cha kumnyang’anya kadi yake ya benki na kuanza kuchukua hela bila kujua password aliipata wapi. “Kuna wakati nilikuwa nataka kumtumia mama laki moja, Madee akanikataza eti kwakuwa watadhani nina hela sana,” anasema. Mpaka tunaongea naye asubuhi hii, anasema kadi yake imebakiwa na shilingi 25,000 tu. Ameendelea kudai kuwa juzi Madee alimpigia simu na kumwambia kuwa kaka yake wa Kibaha ameandaa show ya CCM na atamlipa shilingi laki moja. “Hivi kweli bro mimi ni mtu wa kufanya show ya laki moja?”. Hata hivyo aliamua kukubali ili kuepusha lawama. Baada ya show kumalizika anasema yeye na back up artist wake walirudishwa saa saba usiku wakati asubuhi yake alitakiwa kwenda shuleni kuchukua namba ya mtihani na kuandaa dawati la kukalia. Dogo Janja anaeleza kuwa inamuuma sana kwakuwa muziki haujampa chochote licha ya Madee ambaye huwa hapati hata show kumtumia kimaslahi na hadi leo hii anamalizia kujenga nyumba yake. “Ni kama vile Madee alinipanda ili anivune.” Ameendelea kusema kuwa hiyo juzi sasa hadi kufikia Tip Top watangaze kumfukuza alikuwa kwa Tundaman akipiga story na Madee akamuita kisha kuanza kumpiga. Alichukua simu yake akaondoka nayo. “Jamaa alianza kujitumia meseji kutoka kwenye simu yangu kwenda kwake za matusi ama kuwa nataka kumroga. Jana nimemuonesha >>>>> hizo meseji na amesikitika sana.” Anasema simu yake alipewa jana. Kitendo cha kumwambia Madee kuwa amechoka na anataka kurudi nyumbani ndicho kimemfanya amfanyie yote hayo hadi kumwambia kuwa watahakikisha wanambania asifanye vizuri tena kwenye muziki. Pia amedai kuwa Madee aliwapigia simu wazazi wake ili wamkataze Dogo Janja asifanye interview na vyombo vya habari. “Wanajua nikiongea wataabika sana.”

No comments:

Post a Comment