Thursday, June 14, 2012

Piga simu ya Diva, Imetoka Ule wimbo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu pengine kuliko nyimbo zote mwaka huu wa mtangazaji wa Clouds FM, Loveness aka Diva umeachiwa rasmi jana kwenye internet.Leo unatambulishwa rasmi redioni. Waliokuwa na muda usiku na access ya internet walihaha kuudownload na kusikiliza Je! Yaliyomo yamo kweli? Sisi tumeudownload saa kumi na kitu alfajiri na kuusikiliza kwa makini. Wimbo unaanza kwa sauti ya kimahaba ya Diva iliyoshushwa kidogo kupisha maneno ya producer Lamar ambaye kama kawaida ya nyimbo zake huongea mwanzoni ‘This is the talk of the town blah blah blah’ bila kusahau ‘Exclusive music.’ Diva anaanza kwa chorus yenye maneno ‘nataka kupiga simu kwako wewe wangu baby’ jambo la kwanza linaloweza kukuingia akilini ni ‘Ray C. Yeah, bila kusikiliza sana sauti ya Diva inafanana sana na ya Rehema Chalamila kwenye wimbo huu. Swaggajacking? That’s something she needs to explain by the way!! Anaendela kusikika akisema ‘Pokea simu yangu honey popote ulipo wangu baby’. Lakini baada ya maneno hayo Diva anaamua kudhihirisha kuwa ni kweli Ray C ni role model wake kwa kuyarudia maneno ya wimbo wa zamani wa Ray C ‘Uko wapi’ yasemamayo “Uko wapi nikufuate niambie nikuache, angalau nikuone japo sauti nisikie.” Diamond anaingia kwenye verse ya pili akisikikia, “ Ninapowazaga kamchezo kabaya moyo unanizizima” na kupokelewa na sauti ya kitandani ya Diva (we knew it) oooooohh!! Na Diamond analiokoa jahazi la wimbo huu mfupi kwa kuangusha some good melodies! Mwishoni Diva anamalizia na ‘I love you baby’ na busu refuuuuuuuuuu! So sisi tumeionaje ngoma!!! 50-50! Not bad, not so good! Lakini kwa umaarufu wake na wa Diamond chances are itakuwa hit! And by the way siku hizi you don’t need a good song to make a hit, you need fame, money and promotion to make a hit! Diva anasemaje? “For 2 f--ng hrs zaidi ya watu elf10,500 wame download 'piga simu ... Happiest :-) thanku.” Really? Congrats then. “Kinachouzaga ni melody. Si zaidi .... U know what I mean. Enjoy piga simu. Thanks 4ya support mlioonyesha usiku huu,” aliongeza Diva. Followers wake kwenye twitter wanasemaje? Oooh! Ni rahisi kubashiri…. Lmao. Sifaaaaaa! “OMG! This song is off the hook.....hiyo Sauti Sasa*Am speechless,aiseee* Nice work bibie..... @Divaakamimi *Kissesss!” “Piga cm is such a nice number please play it agin 4me. u know ma precious is away so it reflects much on me here.please diva.” “Yo diva nakupongeza kwakufanya bonge la nyimbo iv ushawah kuimba au h ndo nyimbo yako ya kwanza?”ni cloud charles. “Unajua nn diva!!?we ni mkali sana, umetisha ile mbaya yani mpaka daaah noumer,mtoto pale kati unavyolalamika Mmh,binafsi umenibamba.” “Mimi hahahaha,kaaaliiii..ila ngoja,nimeiskiza kwy simu..subiri niingie hm,i need my Dre beats on...nivumilieni kidooogo nijiridhishe.” (MwanaFA) Wengine nao hawakupenda kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa, “Diamond umejishushia hadhi.mdada gani huyu umeimba naye? anaimba kama vile mjusi kabanwa na mlango, mashairi yenyewe kaiba ya Ray C!” Mwisho, kamwe usidharau nguvu ya mitandao ya kijamii katika promotion ya muziki. Kwa uwezo wake wa kufanya promotion kwa mashabiki wake lukuki, wimbo huu utafika mbali na huenda ukampa hela kama alivyowahi kusema awali kuwa unaweza kutumika kwenye matangazo ya simu.

No comments:

Post a Comment