Thursday, June 14, 2012

Sauda Mwilima afiwa na mtoto wake Mtangazaji wa kipindi cha Bongo Beats cha Star TV amefiwa na mtoto wake wa kiume muda mfupi baada ya kujifungua. Kwa mujibu wa website ya Diamond, Sauda alijifungua mtoto huyo juzi kuamkia jana katika hospitali ya Kinondoni kwa Doctor Mvungi lakini wa bahati mbaya mtoto wake alifariki dunia. Hata hivyo mtandao huo umedai kuwa Sauda bado yupo hospitali na afya yake inaendelea vizuri. Mwezi April mwaka huu, mtangazaji huyo alifunga pingu za maisha na Kauli Juma, katika harusi iliyohudhuriwa na mastaa.

No comments:

Post a Comment