Thursday, June 14, 2012

Roki alienda BBA kusafisha nyota yake ya muziki Shindano la Big Brother Africa siku zote huwa ni jukwaa zuri kwa washiriki kutafuta exposure ya maisha yao ya baadaye. Washiriki wengi hata wale ambao hawakushinda leo hii wako sehemu nzuri na maisha yamebadilika. Wapo waliogeuka watangazaji wa radio ama TV, wapo waliopata deal za matangazo, umodel, movie nk, kutegemea na ushapu wa kila mmoja. Hivyo kila mshiriki huenda mle kwa malengo yake binafsi. Kuna wale ambao huenda wakijua tu kwamba kupata zawadi ya mwisho si kitu rahisi lakini kile kipindi cha miezi kadhaa mjengoni huwapa umaarufu barani Afrika. Ni rahisi kufanikiwa kwa mambo yao baada ya kuwa maarufu. Mwanamuziki wa Zimbabwe Roki anasema aliamua kwenda Big Brother ili kuongeza umaarufu wake. “Walau nikitoka nje ya nyumba hii itakuwa rahisi kwangu kumfuata msanii mwingine wa Afrika kupiga collabo kwakuwa watakuwa wameskia baadhi ya nyimbo zangu zikichezwa hapa na pia kunifahamu.Pia Napata nafasi ya kuwafahamua wasanii wengine wa Afrika.” Lakini kwa msanii huyu, hiyo ni fursa kwake pia kuondoa mtazamo wa mashabiki kuhusu yeye kwakuwa ameharibu CV yake sana huko nyuma.Kuanzia kumshambulia mke wake mpaka kutumikia kifungo cha nje baada ya kupatikana na hatia ya kumiliki bangi na mambo mengine yaliyochafua jina lake. Pia ana watoto watano ambao kila mmoja ana mama yake. Na hao ni wale tu ambao wanafahamika. Kwa kuonekana kwa saa 24 kwenye kamera za BBA meneja wake Bybit Areketa anasema kuwa ni nafasi ya kwake kufufuka tena kwa heshima yake na sio kama mtumiaji wa madawa, mzinzi na mpiga wanawake.

No comments:

Post a Comment