Friday, August 31, 2012

T.I.D MBARONI TENA.MARA HII IKIDAIWA ANATAKA KUMUUA ALI KIBA soma hii hapa.Ally Kiba na T.I.D 
Baada ya kuhojiwa na polisi kwa saa nane,mwanamke ambae anashutumiwa kutaka kumuua Ali Kiba, mwanamke huyo alikiri kwamba alitumwa na T.I.D kwenda kumuua Ally Kiba.
Upande wa pili wa Shilingi haya ndio yaliyosemwa T.I.D amesema “kwa nini nimuue Ally Kiba bwana, si mtu wangu nampenda kabisa bwana, kweli sasa hivi niko polisi kwa ajili ya kuhojiwa, nilikua safari, nimerudi sasa sijui mwanamke gani anaweza kufanya hivyo, siwezi kufanya hivyo, kwa sababu gani? toka nimezaliwa sijawahi kugombana na Ally Kiba, ukibisha muulize mwenyewe kama ameshawahi kukorofishana na mimi,nia ya hao watu ni kuniangusha mimi nionekane ni mtu mbaya nisiuze mziki wangu nisipendwe”
meneja wa Ally Kiba nae amesema haya“hakuna taarifa zozote ambazo ziko tayari kutolewa kwenye vyombo vya habari  kwa sasa hivi  tuwaachie polisi wafanye kazi yao kwanza”
Habari zinazidi kueleza kua mwanamke huyo pamoja na watu wengine ambao wametumwa kukamilisha zoez hilo hawatokei mkoa wa Dar es salaam bali wameingia Dar kwa kaz hiyo tu.Bado Uptowntz inaendelea na umakini wa habari hii kupata tuko hilo zima keep visit us

No comments:

Post a Comment